Diamond Platnumz Ajigamba Kuchangamsha GAME, Awapiga Dongo Hili "Tumieni Nafasi Hii Sinta Wasaidia Tena"



Majibizano baina ya msanii @diamondplatnumz na @officialalikiba yameendelea mitandaoni kisa ushindani mkubwa ulioibuka wa ufuatiliwaji wa nyimbo zao 'ENJOY' na 'SUMU' tangu ziachiwe usiku wa kuamkia Ijumaa.

Baada ya boss wa Kings Music kuibuka na a.k.a mpya ya 'KWEVO' kwenye majibu ya dongo la Diamond, mwimbaji huyo wa 'My Baby' amerudi tena na andiko la kuwataka wasanii wenzake kukitumia kipindi hiki vizuri kwani hatakuwa na huruma hapo baadae dhidi yao.

"Angalau game imechangamka sasa, na mashabiki walipo wana 'ENJOY', sasa msiniangushe jamani, jitahidini kutumia vyema nafasi hii. Mkizembea tena kwa kweli, sitatoa msaada mwingine maana nitachoka kwasababu na mimi ni Mwanadamu".

Kisha amemalizia kwa kusema ataenda zake kuendelea na biashara ya Media kwasababu huko ndiko kuna ushindani halisia.

Diamond ameshirikishwa na @juma_jux kwenye 'ENJOY' huku King Kiba akiwa amempa shavu @marioo_tz kupitia 'SUMU'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad