Diamond Platnumz Alikosea Kurusha Kijembe kwa Wanamuziki wa Bongo Flava..


"Wakati naanza Movements za Kutoka nje ya East Africa wengi mlichelewa kunielewa na mkaanza kusema "Ooh nimeishiwa Utunzi" "Ooh naimba ujinga" na Kashfa kibao, Mkaanza kuwapa vichwa wasanii wasio level yangu washindane nami...kuja Kushtuka nawaletea Matuzo ya Kimataifa na kujaza viwanja kwenye Mataifa ambayo mlizoea Kuyasoma kwenye geography... huku wasanii wenu wakiwa wanasubiri matamasha ya Redio!"---Diamond Platnumz.

Diamond Platnumz ameanzisha Vita, sijui Itakuwaje. Mpaka Sasa Harmonize na Alikiba bado hawajajibu Chochote. Vita bado Mbichi hii.

Binafsi naona Kama Diamond Platnumz hakustahili kuandika Ujumbe huu maana unaonesha kwa kiasi gani anaumizwa anapolinganishwa na Wasanii wengine.

Level ambayo amefikia Diamond sio la kuanza kukumbushia mambo ya Nyuma, akomae atoe ngoma kali akapambane BET huko, Kurushiana Maneno na Wasanii wadogo wa hapa Tanzania wala hakumjengi.

Hivi Sasa ilibidi arushiane Maneno na Burna Boy, Davido au Wizkid ila Sio Wanamuziki wa Ndani ambao kwa sasa ameshawazidi kimuziki, kimaisha, Nakadhalika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad