Mbavu ya kulia ya Yanga SC, Djuma Shaban ipo kwenye mipango na Klabu ya TP Mazembe ya nchini kwao DR Congo.
Imearifiwa kuwa, Yanga tayari wapo kusikiliza ofa ya TP Mazembe kutokana na DJUMA kuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.
Muda wowote kuanzia sasa dili la Djuma na Mazembe huenda likakamilika na urahisi wa Yanga kumuachia unakuja baada ya kukamilisha dili la Yao Khouassi Attohoula.
Djuma kwa sasa anafanya Mazoezi binafsi na hajajiunga na Kambi ya Yanga ya kuanza msimu mpya kwa maana ya Pre Season kule Avic Town akiwa anasikilizia jambo lake litimie.Q