Dk. Slaa: Tuache Unafiki, Vyama vya Siasa Vimegomea Mkutano Wangu…





BALOZI mstaafu Dk. Wilbroad Slaa amewataka Watanzania kuacha unafiki kwani alialika baadhi ya vyama vya siasa kushiriki mkutano unaolenga kujadili mkataba wa uwekezaji bandarini lakini dakika za mwisho vikajitoa. Anaripoti Mwandishi Wetu ..(endelea).

Akimshukuru Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe kwa kukubali kushirikiana naye kuandaa mkutano huo uliofanyika leo Jumapili Temeke jijini Dar es salaam, Dk. Slaa amesema Watanzania wasipoacha unafiki huo Taifa halitakombolewa.

“Ni bahati mbaya na nadhani tuache unafiki Tanzania, tulialika vyama vingine dakika za mwisho wakajitoa, tusipoacha unafiki huu nchi hii haitakombolewa.

“Naomba wanachama wa vyama vyote watambue kuwa wakati wa kukumbatia ambavyo havina masilahi ya taifa wala yenu ni wakati wa kutafakari juu ya vyama hivyo,” amesema Dk. Slaa ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema kabla ya kujiengua ndani ya chama hicho mwaka 2015.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad