Etoo akumbwa na Skendo nzito Cameroon, wataka afungiwe Kisa Betting

Etoo akumbwa na Skendo nzito Cameroon, wataka afungiwe Kisa Betting


Union Movement Sportive (UMS) wameingia kwenye battle dhidi ya Boss wa Shirikisho la soka Cameroon Samuel Etoo kwa kumwita kwenye kamati ya maadili Kwa kosa la kuwa Balozi wa 1XBET


UMS wameomba Etoo afungiwe miaka 6 kujihusisha na soka Kwa Mujibu wa kanuni ya 6&8 ya uendeshaji wa soka.


Hayo yamekuja baada ya Klabu kulalamikia kiongozi wa ngazi ya juu ya FECAFOOT kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri , wakisema kwamba itasababisha upangaji wa matokeo katika Ligi kuu nchini Cameroon


Ikumbukwe Etoo amekuwa Balozi wa 1XBET mwezi uliopita Kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Rigobert Song Kocha wa Indomitable Lion.


Licha ya vuguvugu hilo linaloendelea lakini hakuna tamko lolote lilitolewa na ofisi ya FECAFOOT kuhusiana na mkataba huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad