Exclusive: Asilimia 60 Clotous Chota Chama Kuondoka Ndani ya Simba



Taarifa za uhakika nilizopata kutoka katika chanzo changu ni kuwa Kiungo wa Klabu ya Simba SC,Clatous Chota Chama hana mpango wa kuendelea kusalia ndani ya Kikosi cha Simba SC na mpaka sasa kuna asilimia 60 Raia huyo wa Zambia kuondoka ndani ya Simba SC.

Sababu kubwa za Clatous Chama kutaka kuondoka Simba SC ni kushindwana katika masuala ya mkataba wa kumfanya kuendelea kusalia mitaa ya Msimbazi.

Clatous Chota Chama hajasafiri na Kikosi cha Simba SC katika maandalizi ya pre season Nchini Uturuki.

Mpaka sasa Nyota huyo mezani kuna ofa ya Vilabu vya hapa Nchini na Vilabu vya nje.

Note:Katika Ripoti ya Robert Oliviera "Robertinho " Mwamba wa Lusaka hayupo katika mipango yake kuelekea msimu ujao wa mashindano (2023/2024).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad