Fabrice Ngoma Aliyetekwa na Simba Ashitakiwa FIFA na Al Hilal


MARA baada ya wachezaji wa timu ya Al Hilal kutaka kusitisha mkataba huku wakihusishwa na baadhi ya timu za hapa nchini, mabosi wao wameamua kuwafungulia mashtaka Fifa.

Wachezaji waliositisha mikataba hiyo ni Fabrice Ngoma anayehusishwa Simba, Lamin Jarjou akitajwa Azam FC pamoja na Ibrahim Imoro ambaye bado haijajulika anataka kutimkia timu gani.

Ngoma anadaiwa kusitisha mikataba wake kinyume na taratibu na hiyo kutokuwa na mwanzo mbaya ndani ya timu hiyo kutokana na kuwa na majeruhi wa mara kadhaa.

Kiungo huyo tayari yupo Dar es Salaam akisubiri barua yake ya kumalizana na Al Hilal na wakati wowote anaweza kusaini Simba tofauti na ilivyozushwa kuwa atasaini Yanga au Azam FC.

Wachezaji hao ambao wapo chini ya kocha Florent Ibenge wako njiapanda kwani hatima ya maombi yao ya kusitisha mikataba haijafika tamati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad