Fiston Mayele Aitosa Yanga Safari ya Malawi

 


Mapema leo asubuhi kikosi cha #Yanga kimeondoka Tanzania kwenda nchini Malawi kwenye mualiko maalum wa serikali ya taifa hilo itakapo adhimisha siku ya Uhuru.


Wananchi wakiwa Airport ya Kimataifa ya Mwl. Julius Nyerere waliongozana na usajili wao mpya Nickson Kibabage kwenda kwenye mualiko huo wa heshima.


Hata hivyo wapo baadhi ya Mastaa wao ambao hawakuwepo kwenye msafara huo. @mayelefiston ni miongoni mwa majina makubwa ya #Yanga ambayo waandishi walimtafuta Airport lakini hakuwepo.


Siku za hivi karibuni kumeibuka tetesi zinazomuhusu Fiston Mayele kuondoka Yanga licha ya kuendelea kuboreshewa Mkataba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad