Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Watoa Neno Mkataba Bandari



Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyoketi katika kikao chake cha kawaida leo July 09,2023 Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuitaka Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa Wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari.

Halmashaur Kuu hiyo pia imeazimia kwamba uwekezaji na undeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi na kwamba uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CM ya Mwaka 2020 - 2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92.

Kikao hicho cha NEC, kilitanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi mapema leo.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kauli moja imezipongeza pia Serikali zote mbili za CCM, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutafsiri kwa vitendo llani ya CM ya Mwaka 2020-2025, kwa maslahi na ustawi wa Watanzania wote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad