Hapunguzwi Kazi Mtu Bandarini DP Ikija Kuanza Kazi


Mwenyekiti aliyeongoza Timu ya Mashauriano ya Uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari amesema kwenye makubaliano kuna kifungu kwamba atakapokuja DP World kwasababu yeye teknolojia yake ya juu asilete habari kwamba anapunguza Wafanyakazi bali ni lazima ahakikishe anawatunza Wafanyakazi atakaowakuta.

“Sisi tumeweka kifungu kwamba atakapokuja DP World kwasababu yeye teknolojia yake ya juu asituletee habari kwamba anapunguza Wafanyakazi, tumesema lazima ahakikishe anawatunza Wafanyakazi atakaowakuta, hivyo Bunge limelinda kwa kuridhia hawawezi kutufanyia kama walivyofanya Djibout lakini nashangaa vifungu hivi hamvisemi”

“DP World hatoleta mitambo chakavu kwasababu tumeweka viwango vya mitambo na akienda kinyume tutambana, kuhusu kodi tunatarajia TRA akusanye Trilioni 26 kwa mwaka kwani mifumo mingi itaimarishwa na kuonekana” ——— Hamza Johari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad