.
Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anatarajiwa kuwasili nchini Morocco kesho Jumapili, Julai 26, 2023 kwa ajili ya kukamilisha dili lake la kujiunga na Mabingwa wa Ligi Batola Pro msimu wa 2022/23, AS FAR Rabat.
Kocha huyo raia wa Tunisia amefikia makubaliano binafsi baada ya mazungumzo na klabu hiyo wiki iloyopita.
Taarifa kutoka nchini Morocco zinaeleza kuwa kila kitu kipo sawa kati ya Kocha huyo na Klabu hiyo na atawasili Jumapili ili kuchukua nafasi ya Fernando da Cruz ambaye alifukuzwa Klabuni hapo baada ya kuondolewa kwenye hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kama atasaini Mkataba huo, Nabi atakuwa ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kutoka Afrika ambaye sio raia wa Morocco kuweza kuifundisha AS FAR Rabat.
Nabi ambaye ameipa mafanikio makubwa Yanga msimu uliopita, aliondoka klabuni hapo baada msimu kumalizika akiwa na dili la kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika lakini dili lake hilo lilibuma baada ya kushindwa kufikia makubaliano na mabosi wa Kaizer.
Kwa sasa Nabi yupo nchini kwao Tunisi kwa mapumziko kabla ya kwenda Morocco kuanza majukumu mapya kuelekea msimu ujao