Haya Hapa Maswali, Majibu Kesi Kupinga Kufukuzwa Aanachama kina mdee

 

Haya Hapa Maswali, Majibu Kesi Kupinga Kufukuzwa Aanachama kina mdee

Kesi iliyofunguliwa na waliokuwa wanachama wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya chama chao hicho, kupinga kufukuzwa uananchama huku mjumbe wa bodi ya wadhamini Ahmed Rashid Hamis akiendelea kuhojiwa na upande wa waleta maombi.


Kesi hiyo jana Jumatano Julai 27 ilishindwa kuendelea kutokana na wajumbe wawili wa bodi ya wadhamini, waliotakiwa kuojiwa kushindwa kufika Mahakamani.


Wajumbe hao walitakiwa kuhojiwa ikiwa ni ombi la waleta maombi baada ya wao kumaliza kuhojiwa.


Taarifa iliyotolewa na Wakili wa wajibu maombi, Hekima Mwasipu ilieleza kuwa wajumbe hao; Mary Joachim amepata udhuru anaumwa lakini shahidi mwingine Ahmed Rashid Hamis yuko njiani akitokea Zanzibar


Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dar es Salaam, wakipinga kufukuzwa uanachama kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).


Akihojiwa na Wakili wa Waleta maombi leo Alhamisi Julai 27, 2023 Ahmed (70) amedai alijiunga na Chadema mwaka mwaka 1993.


Amedai amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo Katibu wa wilaya mwaka 1993 lakini hakumbuki hadi mwaka gani.


Amedai baada ya kipindi hicho baadae alikuwa mjumbe wa Baraza kuu, na mjumbe wa bodi ya wadhamini mwaka 2017.


Kuhusu wajumbe wengine wa bodi ya wadhamini wenzake alidai, wapo waliofariki na wengine wameongezeka na kufikia saba.


Hii ni sehemu ya maswali na majibu kati ya Wakili wa waleta Maombi Panya na mjumbe wa bodi hiyo.


Wakili: Nani Mwenyekiti wa Bodi?


Shahidi: Anakaimu kwa sasa Maulida Anna Komu toka 2023


Wakili: Kabla ya hapo alikuwa nani?


Shahidi: Alikuwa Sylivester Masinde ambaye amefariki


Wakili: Unafahamu kwanini upo hapa?


Shahidi: Ndiyo nafahamu ni kwasababu ya shauri la akina Mdee


Wakili: Unafahamu sababu za Chadema kuwafukuza uanachama?


Shahidi: Ni kujiapisha kuwa wabunge bila kuteuliwa na chama


Wakili: Kwa hilo kosa ililosema, Chadema mliwaita kuja kujieleza kwenye kamati kuu na mliwapelekea barua ya wito?


Shahidi: Sina hakika waliitwa vipi?


Wakili: Waliitwa kwa njia zipi?


Shahidi: Sifahamu


Tayari wajumbe wawili wa bodi ya wadhamini ya Chadema, wameshahojiwa akiwemo Ruth Moleli na Profesa Lwaitama.


Wajumbe wengine ni wanaopaswa kuhojiwa ni, Mary Joseph Mush, Maulida Anna Komu.


Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Cyprian Mkeha ambapo waleta maombi wanaendelea kumuhoji maswali ya dodoso mjumbe wa bodi ya wadhamini Ahmed Rashid Hamis.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad