Wakati mastaa wengi wa kigeni wakionekana kushindwa kulimudu soka la Misri, mambo yanaonekana tofauti kwa kiungo Mtanzania, Himid Mao ambaye amefikia makubaliano ya kujiunga na Talal El Gaish inayoshiriki Ligi Kuu Misri, ambayo itakuwa timu yake ya tano kuitumikia tangu alipohamishia majeshi huko miaka mitano iliyopita.
Mao anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji, anajiunga na El Gais akitokea Ghazl El Mehalla aliyoitumikia tangu Septemba 2021.