Huyu Hapa Mrithi wa Mayele, Ni Hatari Mayele 7 Ukiwachanganya Pamoja

 

Huyu Hapa Mrithi wa Mayele, Ni Hatari Mayele 7 Ukiwachanganya Pamoja


 Yanga itakamilisha usajili kwa wachezaji wawili, mmoja wa kigeni na mwingine ni mchezaji wa ndani

Wiki hii Yanga itafunga hesabu zake za usajili kwani dirisha la usajili kwa michuano ya CAF litafungwa Jumatatu ijayo

Baada ya Fiston Mayele kuuzwa, Wananchi wanasubiri kwa hamu ujio wa mshambuliaji atakayechukua nafasi yake

Usajili wa mshambuliaji huyo imeelezwa uko katika hatua za mwisho, Wananchi wakae tayari kumpokea

Hapa tunamzungumzia mfungaji bora wa ligi kuu ya Cameroon 2022/23 Emmanuel Dikongue Mahop kutoka klabu ya Cannon Younde akimaliza msimu na mabao 15, assist 3

Kwa kuzingatia mahitaji ya Yanga msimu ujao, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amepambana kwelikweli kuinasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye timu nyingi zimehitaji huduma yake

Mahop ana kasi, nguvu na maarifa ya kuwatoka mabeki. Anatumia vyema miguu yake yote miwili akiwa miongoni mwa washambuliaji wa timu ya Taifa ya Cameroon (sio ile ya CHAN)

Kabla ya kutua Cannone Younde, Mahop aliitumikia Fc Akonagui ambapo katika msimu wa 2019/20 alipachika mabao 24 na kutoa assist 5

Huyu ni mchezaji sahihi kuvaa viatu vya Mayele anayesubiri kutangazwa na klabu ya Pyramids Fc ya Misri

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad