Inshu ya Chama Kugoma Kwenda Uturuki na Simba, Unaambiwa Anatingisha Kiberiti ana Offer Kubwa Mkononi

Kiungo Clatous Chota Chama
 

Kiungo Clatous Chota Chama hajasafiri na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC kuelekea Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season) na kwa mujibu wa CEO wa klabu hiyo Imani Kajula kiungo huyo ana matatizo binafsi.


Hata hivyo inaelezwa matatizo ya mkataba ndio sababu ya Mwamba wa Lusaka kubaki Nchini na inadaiwa mkataba wake na Simba SC ulifikia ukomo mwisho wa msimu uliopita 2022/23.


Kwa mujibu wa vyanzo Chama ameuambia uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi kuwa anahitaji maongezi na ana ofa mkononi lakini alipoambiwa aseme ofa inatoka wapi 'The Triple C' amewaambia viongozi jambo hilo ni siri yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad