Jemedar Said: Usajili wa Yao Yanga ni kwa ajili ya Kapombe

 

Jemedar Said: Usajili wa Yao Yanga ni kwa ajili ya Kapombe

Yanga wanafanya maboresho katika baadhi ya maeneo ya kikosi chao na miongoni mwa meoeneo hayo ni eneo la beki wa kulia.


Yanga tayari wameshusha beki kutoka ASEC Mimosas Yao Kuoassi Attoula lakini mara baada ya utambulisho huo ulioibua furajha kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga.


Mchambuzi wa Michezo kutoka kituo cha EFM, Jemedari Said kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika andiko ambalo limeonekana kuwachanganya wapenzi wengi wa Soka nchini.


Jemedar ameandika;


"Ujio wa Kibwana Shomari na baadae Djuma Shaaban ulionekana kama ulikuja kuua utawala wa Shomari Kapombe wa Simba SC ambaye amekuwa kinara eneo la mlinzi wa pembeni kulia kwa karibu miaka (misimu) 10 sasa hapa Tanzania kwenye Ligi Kuu."


"Wakati anatambulishwa DJUMA SHAABAN ilisemwa “Mwanajeshi wa Bemba” huyo ni zaidi ya mara 100 ya Shomari Kapombe wa Simba SC."


"Misimu 2 baadae ripoti ya kocha mkuu wa Yanga aliyeondoka katika ripoti anatamka kwamba eneo la ulinzi wa pembeni kulia linahitaji mtu jadidi. Hii maana yake ndo kwamba waliopo wana mchango lakini haukidhi haja, haujafikia ule wa Kapombe."


"Ukweli usionenwa ni kwamba KAPOMBE amekuwa kipimo cha mabeki wengi wa pembeni kulia wanaonaosajiliwa nchini, swali linakuwa anamzidi Kapombe?"


"Yao Kuoassi Attoula anakuja kupambana na mfupa uliomshinda Djuma Shaban, Israel Mwenda, Duchu, Chilambo, Kibwana, Lusajo,


na wengine wengi ambao wamecheza ulinzi wa pembeni kulia kwenye Ligi Kuu"


Je Mwananchi unadhani Yao Kuoassi ameletwa kushindana na Kapombe? Tuachie maoni yako


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad