Jezi ya Simba Kuzinduliwa Mlima Kilimanjaro, Ahmedy Ally Awafungukia Wanaobeza



Ameandika Haya Ahmedy Ally:

Jana walikua na tukio lao lakini ghafla wakaacha kujadili jambo lao wakanza kujadili Uzinduzi wa Jezi zetu Mlima Kilimanjaro

Hii ndo maana kutengeneza Agenda, na Agenda inatengenezwa na watu wakubwa ambao ndo sisi

Lakini pia lengo letu la kuutangaza Mlima Kilimanjaro na kuzitangaza Jezi zetu limefanikiwa kwa asilimia mia moja

Ajabu ni kwamba hadi ukurasa rasmi wa klabu umeingia mkenge na kujadili tukio letu

Ukweli ni kwamba watu wengi wameshapeleka Jezi Mlima Kilimanjaro, lakini hao ni watu binafsi waliofanya kwa Utashi wao

Hii yetu ni kitu rasmi na ina baraka ya Mamlaka zote na kubwa zaidi ni dunia nzima sasa inajua kuwa Jezi ya Mnyama itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro

𝐇𝐢𝐢 𝐢𝐦𝐞𝐰𝐚𝐢𝐧𝐠𝐢𝐚

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad