Jose Chameleone Hoi Taabani, Anaumwa Sana, Baba Mzazi Afunguka

 


Baba mzazi wa mwimbaji Jose Chameleone, Mzee Gerald Mayanja amethibitisha kuwa mtoto wake anaugua ugonjwa wa ajabu wa tumbo ambao umekuwa ukimlaza kitandani wiki chache zilizopita.


Wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na Bukedde TV Baba yake Chameleone aliweka wazi kuwa mwanawe amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya tumbo tangu ahamie nchini Marekani.


“Chameleone amekuwa mgonjwa katika miezi iliyopita. Alipohamia Amerika, ugonjwa ulizidi kuwa mbaya. Sasa ni mgonjwa sana, yuko kwenye kitanda chake cha wagonjwa. Amekuwa akipata matatizo ya tumbo ila kwa sasa anapokea matibabu,” alisema Mzee Gerald Mayanja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad