Kanye West ameanza kutengeneza mipango kwa ajili ya Kampeni za mwaka 2024, kuwania kiti cha Urais wa Marekani.
Kwa mujibu wa HipHopDX, kupitia Documentary iitwayo ‘The Trouble with KanYe’ rapa huyo na mfanyabiashara alikutana na jamaa aitwaye Mark ambaye hana makazi (homeless) na amekuwa akiishi kwenye gari lake nje ya Kanisa ambalo YE amekuwa akienda.
Baada ya kukaa chini na kubadilishana mawazo, YE alimuona Mark kuwa mtu mwenye mtazamo tofauti na anaweza kujenga hoja kutokana kuchangia vizuri kila mada ambayo walikuwa wakiizungumza, sasa basi YE ameamua kumpitisha jamaa huyo kuwa meneja wa Kampeni zake kwenye kuwania Urais wa Marekani mwaka 2024.