Kesi ya Chadema na Wabunge 19 Waliofukuzwa Uanachama Kuendelea Leo



Kesi hiyo inarejea tena Mahakamani leo Julai 10, 2023 baada ya kusimama kwa siku 54 (Tangu Mei 17, 2023) ilipoahirishwa kutokana na Jaji Cyprian Mkeha anayesikiliza Kesi hiyo kwenda kwenye Semina ya Majaji

Kesi hiyo inayohusu uhalali wa utaratibu uliotumika kuwavua Uanachama Wabunge 19, kuna hatua ya mahojiano kati ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Mawakili wa Wabunge hao akiwemo Halima Mdee

Halima Mdee na wenzake 18 wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu iliyowafuta uanachama Novemba 27, 2020 kwa tuhuma za kuapishwa kuwa Wabunge bila ridhaa ya Chama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad