Kibegi cha Simba Chawa DILI, kupigwa mnada wiki hii

 

Kibegi cha Simba Chawa DILI, kupigwa mnada wiki hii

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamesema wanatarajia kukipiga mnada kibegi cha jezi ambacho kilipanda Mlima Kilimanjaro kwa jili ya uzinduzi wa jezi za msimu mpya wa 2023-24.


Akizungumza leo Julai 25, 2023 kwenye mkutano wa waandishi wa habari, CEO wa Simba Imani Kajula alisema kibegi hicho kitapigwa mnada na fedha zitakazopatikana, zitatolewa msaada.


"Wiki hii tunatarajia kufanya mnada wa kibegi pamoja na jezi zile na mapato yake yatasaidia ujenzi wa wodi ya kina mama na mtoto kwenye hospitali ya Muhimbili na Zanzibar," alisema CEO Imani Kajula.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad