KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis Amejihakikishia Nafasi Simba


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis amejihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha msimu ujao, licha ya maingizo mapya ya wachezaji wanaocheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Simba imewasajili viungo washambuliaji wanne wa kigeni ambao watakuwa na kibarua ya kumpoka namba Kibu aliyejihakikishia nafasi ya kucheza katika msimu uliopita chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oliviera Robert ‘Robertinho’ ambaye kipenzi chake.

Viungo hao washambuliaji waliosajiliwa na Simba ni Aubin Kramo, Willy Onana, Fabrice Ngoma na Luis Miquissone aliyetambulishwa wikiendi iliyopita huko kambini Uturuki.


Willy Onana

Kibu juzi aliibuka shujaa katika mchezo wa kwanza wa kirafiki ambao Simba walicheza dhidi ya Zira FC ya nchini Uturuki na kuifungia bao moja katika sare ya bao 1-1.

Akizungumza na Championi Jumatano, kiungo wa zamani wa Taifa Stars na klabu za Simba, Yanga na Azam FC, Amri Kiemba alisema kuwa ngumu kwa Kibu kuondolewa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, licha ya maingizo mapya ya wachezaji.
Kiemba alisema kuwa, kiungo huyo ana faida kubwa katika soka la hivi sasa, ni mchezaji mwenye kasi akiwa na mpira akishambulia goli la wapinzani.

Aliongeza kuwa anaamini kama kiungo huyo hataanza katika kikosi cha kwanza, lakini ngumu kwake kukosa nafasi ya kushiriki katika kila mchezo ambao Simba watauchea mbele ya viungo hao wapya.

“Lipo wazi kabisa kwa aina ya uchezaji ambayo anayo Kibu, hawezi kuwa mnyonge hatakama kuna maingizo mapya kiasi gani bado atapata nafasi ya kucheza.
“Ninaamini hatakama atakosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, lakini hawezi kukosa nafasi ya kucheza katika kila mchezo kwa maana ni mchezaji ambaye anaendana na mahitaji ya aina ya soka la kisasa.

“Hivyo viungo hao wapya wana kibarua kigumu mbele ya Kibu ambaye yeye apewi thamani kubwa, licha ya mchango mkubwa ambao amekuwa akiutoa Simba,” alisema Kiemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad