Kumbe Jonas Mkude Sio Jezi Namba 6 wa Yanga Wanayotumia Kuwajambisha SIMBA, Ally Kamwe Afunguka

 


Joto likiwa linazidi kupanda kwa Mashabiki wa Soka nchini wakitaka kumjua mchezaji atakaeva jezi namba 6 ya Yanga ambayo ilikuwa ikivaliwa na Feisal Salum alietimkia Azam FC.

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe ameweka wazi siku ya utambulisho wa mchezaji huyo na sifa zake kuelekea kilele cha Siku ya Mwananchi ambayo itakuwa Julai 22.

“Hadi kufika Jumanne, tutakuwa tumemaliza zoezi zima la utambulisho wa sajili zetu.Watu wanafikiri utambulisho wa Jonas Mkude ndio namba 6 tuliyoisema, bado namba sita hajatangazwa,”

“Yeye atakuwa ni mtu wa mwisho kutangazwa, siku akitangazwa wananchi wataingia mtaani kufurahia, itakuwa ni kama sikukuu ya mwaka mpya.Tukimtambulisha mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi,”

“Tutamtambulisha kabla ya wiki ya Wananchi, Kaizer Chiefs wao watakuwa watu wa mfano kuwasimulia watu wengine kuhusu unyama na ukatili alionao huyu jezi namba 6.”

Mpaka sasa Yanga imeshafanya usajiliwa wachezaji watano wazawa wawili na wa kigeni watatu ambao ni Nickson Kibabage, Jonas Mkude (wazawa) na wa Kimataifa ni Beki Gift Fred, Maxi Mpia Nzengeli na beki Yao Khouassi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad