Kweli Simba ni Baba Lao..Hotel Watakayofikia Uturuki Hii Hapa, ni ya Mastaa Wakubwa tu

 

Kweli Simba ni Baba Lao..Hotel Watakayofikia Uturuki Hii Hapa, ni ya Mastaa Wakubwa tu

KWA Lugha rahisi unaweza kusema kambi ya Simba wanayokwenda kuiweka nchini Uturuki ni ya kifahari wakiwa wanajiandaa na msimu 2023/24 ambao wamepanga kufanya maajabu Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Simba wanatarajia kuondoka nchini Julai 11, mwaka huu kuelekea nchini humo kujikita kwa wiki tatu kabla ya kurejea katika ardhi ya Tanzania kwa ajili ya Tamasha lao la Simba Day, na baadae kuanza mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara na CAF Super League.

Akizungumza na jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmed Ally ambaye ameweka wazi kwamba, watafikia hoteli ya kifahari yenye kila kitu ndani kwani wanao uwezo wa kifedha pia kukidhi mahitaji ya benchi la ufundi linaloongozwa na Roberto Oliviera (Robertinho).

Alisema mapendekezo ya kocha huyo kupata muda wa wiki tatu hadi nne kwa ajili ya kukaa na wachezaji wake katika mazingira mazuri yenye utulivu kwa ajili ya kaandaa timu iliyo imara.

“Nadhani mmeona taarifa yetu kwamba tunaelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kuelekea msimu unaokuja, Kila kitu kimewekwa vizuri na Kocha Robertinho amewashawasili nchini akiwa na baadhi ya wasaindizi wake.

Kikosi kitaondoka nchini Julai 11, mwaka huu baada ya wachezaji wote, walikuwepo tangu awali na wapya watakuwa wamewasili kabla ya Julai 11, mwaka huu na kuwepo katika msafara huo,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa watafikia hoteli ya kifahari, yenye kila kitu ndani ikiwemo uwanja na miundo mbinu yote ya kisasa ya kufanyia mazoezi kwa timu hiyo watakapokuwa nchini humo.

“Simba ni timu kubwa ambayo haiwezi kufunga safari mpaka Uturuki halafu tufikie hoteli ambayo haina mbele wala nyuma, lazima tuwaweke wachezaji wetu mahali mazuri, penye hadhi ya timu kubwa kama Simba,” alisema Ahmed.

Alieleza kuwa watakapokuwa nchini humo watacheza mechi tatu za kirafiki licha ya kutojua watacheza na timu gani hadi hapo watakapofika nchini humo.

Kuhusu usajili, Ahmed ameshusha presha za masabiki hao kuwaambia asilimia 80 ya wachezaji waliokuwa wanahitajika kwa msimu wa 2023/24 wameshamalizana nao.

Licha ya kutoweka wazi juu ya wachezaji wapya wanawasili lini  taarifa zinasema  kuwa tayari nyota hao waneanza kuwasili tangu usiku wa jana akiwemo kipa wao mpya raia wa Brazil, Caique Luiz Santos da Purificacao anbaye alitua nchini na Kocha Robertinho.

Baadhi ya nyota wanaotajwa ni Willy Onana kutoka klabu ya Rayon Sport ya Rwanda, Beki Mcameroon Che Fondoh Malone, Milton Karisa kutoka Vipers ya Uganda, Yahya Mbegu kutoka Ihefu FC na Efoe Nova kutoka klabu ya Asko Kara.

JEZI ZA MSIMU MPYA HIZI HAPA.

Kampuni ya Sunderland imesema itazindua kwa pamoja jezi zote za Klabu ya Simba za mashindano ambayo wanashiriki kwa msimu wa 2023/24.

Jezi hizo ni za CAF Super League, Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Ligi Kuu ya Wanawake na Ligi ya Vijana.

Akizungumza na Azam TV, mzabuni aliyeshinda zabuni ya kutengeneza jezi za Simba SC, Sunday Omar amesema tayari jezi hizo zipo nchini na klabu ndio watasema wanazindua lini.

Amemuomba Waziri wa Biashara na Viwanda, Mkurugenzi wa FCC, Polisi na mamlaka nyingine kusaidia kudhibiti jezi ‘Fake’ ili timu zinufaike na mapato yanayotokana na mauzo ya jezi zao.

Sunderland iliingia mkataba Sh bilioni 4 na Simba SC baada wa miaka miwili wenye thamani ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia nao miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh bilioni 2.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad