Ligi ya Mabingwa Afrika Simba Kuanza Round ya Pili, Yanga Round ya Kwanza




Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa, #Simba itaanzia Raundi ya Pili kwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya Power Dynamos (Zambia) dhidi ya African Stars (Namibia)

#Yanga itaanzia Raundi ya Kwanza kwa kukipiga na ASAS ya Djibouti, timu itakayoshinda itaingia Raundi ya Pili na kukutana na timu itakayoshinda kati ya Otoho ya Congo dhidi ya Al Merrikh ya Sudan

#KMKM ya Zanzibar itaanzia Raundi ya Kwanza kwa kukipiga na #StGeorge ya Ethiopia, mshindi wa hapo atacheza dhidi ya Bingwa Mtetezi #AlAhly ya Misri

Mechi za Raundi ya Kwanza zitachezwa Agosti 18–19 na marudio ni Agosti 25–26, 2023, Raundi ya Pili ni Septemba 15–16 na marudio ni Septemba 29–30, 2023, baada ya hapo inafuata Hatua ya Makundi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad