Madawa ya Kulevya Aina ya Cocaine Yakutwa Ndani ya Ikulu ya Marekani




Uchunguzi wa awali wa “poda nyeupe” iliyopatikana katika Ikulu ya Marekani umeonesha kuwa poda hiyo ni dawa ya kulevya aina ya cocaine.


Cocaine hiyo kwa sasa imepelekwa maabara kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi, inaarifiwa kuwa kupatikana kwa cocaine hiyo Ikulu kulisababisha hali ya taharuki na kama njia ya tahadhari Watu walihamishwa kutoka kwenye jengo hilo kwa lengo la kuimarisha usalama.


Ripoti za awali zimeonesha kuwa dawa hizo ziligunduliwa katika maktaba ya marejeleo huku ikidaiwa kuwa imepatikana katika eneo linalofikiwa na vikundi vya Watalii, sio katika ofisi yoyote ya West Wing.


Wakati wa kubainika kwa cocaine hiyo Rais Joe Biden alikuwa mapumzikoni Camp David akiwa na Mke wake Jill Biden jijini Maryland na kurejea Ikulu ya Marekani asubuhi ya jana.


Hii haitokuwa habari ya kwanza ya dawa za kulevya kuhusishwa na Ikulu ya Marekani kwani mwaka 2013 kuliibuka gumzo baada ya Rapper Snoop Dogg kunukuliwa akisema alivuta bangi ndani ya choo cha Ikulu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad