Maisha Ya Ulaya na Marekani ni Magumu Msikimbilie Huko...Mwamba Huyu Hapa Atoa Ushuhuda



Modest Bafite aelezea uzoefu wake kuhusu maisha ya Ulaya na America kwa wale wenye ndoto za kwenda kutoboa huko

"Hivi umewahi kujiuliza ni kwanini watu weusi wengi tunadhani kuzamia nchi za watu au kuishi katika nchi za nje ni kufanikiwa maisha?? Leo ntakupa sababu, halafu ntakupa uhalisia wa maisha Ya Ulaya na Marekani.

Sababu moja kubwa ni sisi ambao tumebahatika kwenda huko au kuishi huko ni kwamba hatuwaambii watu ukweli na uhalisia badala yake tuna-brag(kuringishia) kuwa tumetoboa.

Nina ukweli usiopingika kwamba ughaibuni ni kuzuri sana na unaweza ukafanikiwa endapo utakuwa unaishi kihalali, Umesoma, Una kazi yako nzuri na ukaishi kwa malengo zaidi.

Wengi hamfahamu kuwa maisha ya Ulaya na Marekani ni magumu mno mno, kuna watu hawana hata pa kuishi, wako kama machokoraa, wanalala barabarani, wanaombaomba, kuna wanaouza vitu barabarani kama wamachinga, kuna wanaoishi huko kwa misaada ya Serikali tu. Wenye nchi zao wenyewe wanahangaika ije kuwa sie tunaoenda tutoboe kirahisi tu kakwambia nani??

Mtu anaenda huko eti mwaka 1 au 2 anaambia watu kafanikiwa, labda kama ana miujiza yake huko. Kufanikiwa ukiwa ughaibuni kunahitaji muda haswa tena sio muda wa kitoto, tatizo wengi wanaoishi ughaibuni wakipost mitandaoni hivi vitu huwa hawaonyeshi, na huwa hawasemi ukweli, wao huonyesha kasehemu kadogo sana ka maisha yao ambako kanaonesha tu kuwa wanakula bata

Amini usiamini tuliotembea tunalijua hili fika. Tofauti ya maisha yetu Afrika na huku ughaibuni, ni miundombinu yao mizuri, teknolojia iko juu sana, system nzuri ya Serikali iliyoweka kusaidia raia wake na uchumi wao kuwa juu, ndio maana dola, euro au pound 100 ni mara 2 mpaka 3 ya pesa ya huku, ila ukweli ni kwamba hiyo pesa ni ndogo sana sana huko kwao, ila kwetu Afrika ni kubwa.

Watu huko wanafanya kazi kule kama mashine, hakuna kujivutavuta kama Afrika, mtu anafanya kazi 2 mpaka 3 ili à-survive, imagine kazi moja tu inavyokuchosha, Sasa kuanya kazi kama hizo 2, Kuna watu wanalala masaa mawili yakizidi ni matatu masaa mengine yote ni kazi, sio kwamba wanatafuta utajiri, ila wanatafuta hela za Bills

2........"Usije ukapumbazika mtu akikwambia huko analipwa dola au euro au pound ukaona pesa nyingi sana lakini kiuhalisia kule si kitu yaani ni pesa ya karanga tu. Waliofanikiwa wengi hujitahidi kuweka akiba ambayo wanakuja kuwekeza nchini kwao sababu pesa hiyo kwa huku walau inaweza kufanya kitu, na ili ufanikiwe pia Lazima uwe umesoma,

Ikumbukwe elimu yako ya Afrika haina kazi huko, inaweza kukusaidia tu badala Ya kusoma labda kwa Miaka 10 ukasoma kwa Miaka miaka.mitano, hii itakusaidia kupata kazi Nzuri inayolipa vizuri, usipokuwa tayari kusoma kwa asilimia 95 utaishia kufanya kazi kama punda viwandani.

#Mytake : kama una nafasi ya kufanya kitu nchini mwako basi komaa na unaweza kufanikiwa zaidi hata ya wanaoishi Ughaibuni.
Kuna watu huwa wanaenda huko, wanarudi nchini kwao wamechoka na hawana kitu chochote, na wakati huo wanawakuta wale waliosoma nao au wa karibu yao wamefanikiwa kuwazidi . Hivyo unaweza kupambana nyumbani na ukatoboa.

Ila endapo ukipata nafasi ya kwenda Ughaibuni kutafuta maisha ni sawa kuchukua hiyo fursa lakini hakikisha iwe kihalali na katafute kwa malengo. Watu wamepoteza maisha huku hata ndugu zao hawajui, watu wanarudi na magonjwa ya ajabu na wengine wamekua mashoga/wasagaji kwa kutaka mtelezo.

Ndugu zetu tuliopo ughaibuni nawaasa, tuache ku-fake maisha, acheni kabisa kwasababu mnapotosha watu kuwa huku maisha ni rahisi sana na kufanikiwa ni nje nje,

Narudia tena, kufanikiwa unajibu ni sio rahisi hata kidogo, Labda kama unaishi kihalali, na umesoma halafu ukawa na malengo thabiti, hapo kutakuwa na urahisi flani, na sio chini Ya Miaka 5,10 kuendelea, usitegemee kutoboa ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu maana haiwezekani.

Kama kuna ulilojifunza, chukua hiyo🙌"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad