Majembe Benard Morrison, Yannick Bangala Wanawindwa Singida Fountain Gate

 

Majembe Morrison, Bangala Wanawindwa Singida Fountain Gate

Uongozi wa Singida Fountain Gate umesema kuwa wanatamani kuwa na kiungo Mkongomani Yannick Bangala na Mghana Bernard Morrison kwa ajili ya msimu ujao huku ukipanga kuweka wazi kila kitu hivi karibuni.


Wachezaji hao wanahusishwa kutua Singida Fountain Gate kwa ajili ya msimu ujao ambao watashiriki Michauno ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.


Young Africans tayari imetangaza kuachana na Morrison huku ikitajwa Bangala huenda ikamtoa kwa mkopo.


Mtendaji Mkuu wa Singida Fountain Gate, Olebile Sikwane amesema kuwa wanatamani viungo hao wawepo nao katika msimu ujao wakiamini wataongeza thamani ya timu hiyo.


Sikwane amesema kuwa hadi hivi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya viungo hao na Singida Fountain Gate.


Ameongeza kuwa hatima ya viungo hao kuichezea timu hiyo, itajulikana hivi karibuni mara baada ya taratibu kukamilika.


“Tunakwenda katika michuano mikubwa Afrika ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, hivyo tunatamani tungekuwa na viungo hao.


“Ipo wazi Morrison yupo katika kiwango kikubwa ni kati ya viungo ambao wangekuja kuifanya Singida Fountain Gate imara. “Pia Bangala ni kati ya viungo bora hivyo tunaamini kuwa akipatikana yeye na Morrison watakuja kuipa thamani timu yetu,” amesema Sikwane

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad