Mama Diamond Platnumz Ajiachia na Koffi Olomide

 

Mama Diamond Platnumz  Ajiachia na Koffi Olomide

Mama Dangote amewaacha mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram wakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu baada ya kupakia video akiwa na msanii wa muda mrefu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide.


Katika video hiyo, wawili hao walionekana wakipiga misele ndani ya jumba moja la kifahari huku wakichukua muda wao kupigwa picha na mlinzi wa Olomide.


Mama Dangote alipakia video hiyo na wimbo ambao ulisikika ukiimba ni ule wa mwanawe, msanii Diamond Platnumz akimshirikisha Chike kutoka Nigeria, wimbo ambao umezaliwa siku moja iliyopita – My Baby.


Baadhi walihoji wawili hao walikuwa wakizungumza nini ikizingatiwa familai hizo mbili zina urafiki wa muda sasa tangu Diamond amshirikishe Koffi katika wimbo wa Waah ambao ulivunja rekodi nyingi ndani ya kipindi kifupi.


Mashabiki wengine walitania kwamba wawili hao walikuwa na lugha gongana baina yao kwani Koffi pengine hana ufasaha katika Kiswahili na wakati huo huo pia mama Dangote hana weledi sana katika Kiingereza wala Kifaransa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad