Marioo Atoa Kauli Chino kushindanishwa na Diamond Platnumz "Msimpe Kichwa Dogo"

 

Marioo Atoa Kauli Chino kushindanishwa na Diamond Platnumz "Msimpe Kichwa Dogo"

 Marioo Atoa Kauli Chino kushindanishwa na Diamond Platnumz "Msimpe Kichwa Dogo"

Msanii wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu dancer wake ambaye pia ni msanii wa muziki, Chino ambaye kwa sasa ana-trend huku akishindanishwa na Diamond Platnumz.


"Ninafurahi namna ambavyo watu wamempokea Chino, huyu ni kijana wangu pale Bad Nation, mimi ndio mtu wa kwanza kumwambia fanya hiki kitu baada ya kuona kipaji chake, alikuwa akiimba sana nyimbo zangu nikaona huyu ana kitu.


"Chino sio kama dancers wa zamani, ana kipaji na aweza kufanya kitu watu wakamsikiliza, kwa hiyo alivyoanza kufanya nikasema ni jambo zuri. Bad Nation ina dancers wengi sio Chino pekee, wote wanafanya vizuri.


"Management nyingi zinakuja zikimuhitaji Chino, nikiona amepata nafasi kubwa zaidi nitamuachia afanye mambo yake. Hata ikitokea mimi nina shoo nay eye ana shoo, kama anapata riziki kuwa basi nitamuachia akafanye mimi nitaenda na hawa wengine.


"Nachoshukuru ananiheshimu nimamshauri pia vitu vya kufanya na ninapenda kuona afanye makubwa zaidi.


"Kushindanishwa na Diamond naichukulia kama utani, Diamond yupo kwenye game muda mrefu na ana biashara yake, kila mtu anajua kama ni suala la utani. Chino ni mtu wa masihara sana lakini anajua anachokifanya.


"Sidhani kama Chino kwa sasa anaweza kushindana na wasanii wakubwa ambao wapo kwenye game muda mrefu," amesema Marioo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad