Maswali ni Mengi, Wapi Walipo Hawa Miamba?

 

Maswali ni Mengi, Wapi Walipo Hawa Miamba?

Ni suala la muda tu kwa mastaa wa Yanga Djuma Shaban na Yanick Bangala kupewa mkono wa kwa kheri ndani ya timu hiyo baada ya namba za jezi walizokuwa wakizitumia zikipewa mastaa wapya kuonyesha ndo imetoka hivyo.


Wachezaji hao ambao kila mmoja amedumu kwa misimu miwili hawapo kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Kigamboni huku namba za jezi zao wakipewa wachezaji wapya.


Namba 4 aliyokuwa akiitumia Bangala kwa sasa amepewa beki Kouassi Yao anayemudu pia kucheza kama winga huku kiungo Pacome Zouzoua akichukua namba ya Djuma namba 21.


Mbali na mastaa hao wapya pia beki Nickson Kibabage aliyekuwa anakipiga Singida Fauntain Gate amepewa jezi namba 33 iliyokuwa ikivaliwa na winga Mghana Bernard Morsson aliyepewa 'Thank You' mapema baada ya mkataba wake kumalizika.


Pia, kwa upande wa Jonas Mkude aliyekuwa Simba na kusajiliwa na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja ombi lake la kuvaa jezi namba 20 limegonga mwamba na sasa atavaa namba 22 baada ya mwenye namba yake, Zawadi Mauya kuchomoa kumuachia kama alivyoomba Nungunungu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad