Matokeo ya mechi ya kirafiki Zira Fc vs Simba Leo July 23






 Mchezo wa kwanza wa kirafiki katika pre-season ya Simba huko Uturuki dhidi ya Zira Fc, umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Simba ilikuwa ya kwanza kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Kibu Denis aliyemalizia pasi murua ya Saido Ntibazonkiza


Bao la Zira Fc inayoshiriki ligi kuu ya Azerbaijan, lilifungwa na Rustam Ahmadzade

Katika mchezo huo Simba ilianza na Ali Salim, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Hennock Inonga, Che Malone, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Sadio Kanoute, Moses Phiri, Saido Ntibazonkiza na Willy Onana

Katika kipindi cha Aubin Kramo aliingia kuchukua nafasi ya Phiri, Clatous Chama akaingia nafasi ya Onana, Bocco akaingia kuchukua nafasi ya Kramo aliyepata majeraha, Fabrice Ngoma akaingia nafasi ya Sadio Kanoute na Isarael Mwenda akaingia nafasi ya Kibu Denis

Huu ni mchezo wa kwanza wa kujipima kwa Simba baada ya wiki mbili za mazoezi huko Uturuki

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad