Web

Mbunge afariki kwa ajali ya Pikipiki, RC Mbeya, anena ‘Alikuwa akielekea shambani kwake’

Top Post Ad



Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM), Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Fransis Leonard Mtega amefariki Dunia mchana wa leo baada ya kupata ajali ya pikipiki akiwa anaelekea shambani kwake.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema “Mtega amefariki kwa ajali ya pikipiki iliyokuwa imembeba ambayo imegongana na trekta (Power Tiller)”.

Homera amesema mwili wake Mbunge huyo utaondolewa Hospitali ya Chimala na kupelekwa Hospitali ya Rujewa inakopatikana huduma yenye jokofu huku akiahidi kutoa taarifa zaidi baadaye “Kuna wanaosema pikipiki alikuwa anaendesha mwenyewe, wengine wanasema alipakiwa lakini asilimia kubwa wanasema alikuwa anaendesha mwenyewe, tunafuatilia zaidi.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.