Mbunge aliyefukuzwa Chadema aibuka mkutano CCM






MBUNGE Viti Maalum, aliyefukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jesca Kishoa, ameibuka katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka wananchi wameuunge mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akisema anaiendesha nchi vizuri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida…(endelea).

Tukio limetokea jana tarehe 23 Julai 2023, mkoani Singida baada ya Kishoa kupewa nafasi ya kusalimia wananchi walioshiriki mkutano wa hadhara uliokuwa unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.


Kabla hajahutubia mkutano huo, Kishoa aliwasalimia wananchi waliofika katika mkutano huo kwa kuwaambia “kidumu Chama Cha Mapinduzi, CCM) hoye”, ambapo alijibiwa.

“Mungu ametupendelea sana kutupa Rais mvumilivu, Nataka niwaambie tumependelewa sana na Mungu amempa uvumilivu kutokana na yanayoendelea, amekuwa Rais wa mfano kuendeleza sekta zote nchini. Mimi binafsi napendezwa sana na Rais na namuunga mkono,” alisema Kishoa.



Kishoa pamoja na wabunge wenzake 18 wakiongozwa na Halima Mdee, walifukuzwa Chadema Novemba 2020, kufuatia msimamo wao wa kukubali kuapishwa kushika wadhifa huo, ikidaiwa ilikuwa kinyume na msimamo wa chama chao.

Baada ya kufukuzwa, wabunge hao wametinga Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa Chadema, kwa madai kuwa uamuzi haukuwa halali kwa kuwa hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.

Kesi hiyo inaendelea mahakamani hapo mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, ambapo wanaomba mhimili huo ufanyie mapitio dhidi ya mchakato uliotumika kuwavua uanachama kama ulikuwa halali au la.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad