Mchambuzi Ngereza"Benard Morrison ni Bora Kuliko Skudu Uwanjani"

 

Mchambuzi Ngereza"Benard Morrison ni Bora Kuliko Skudu Uwanjani"

Mchambuzi wa soka kutoka kituo cha runinga cha TV3, Alex Ngereza amedai kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mahlatse Skudu Makudubela hana kiwango kumzidi aliyekuwa winga wa timu hiyo, Bernard Morrison.


Ngereza amesema hayo ikiwa ni siku moja mara baada ya Yanga kumtambulisha Skudu raia wa Afrika Kusini ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya Marumo Gallants.


"Morrison ni Bora kuliko Skudu, kilichomuondoa Morrison Yanga ni sio uwezo Bali ni nidhamu, Skudu hana uwezo kama wa Morrison na amesajiliwa na Yanga Kwa sababu hana matukio mengi ya nje ya Uwanja," amesema Alex Ngereza.


Skudu anafahamika zaidi kwa machachari yake ya kuchezea mpira na chenga kwa wapinzani wake kama ambavyo alikuwa akifanya Morrison.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad