Mchezo wa Yanga vs Kaizer Chiefs Kuoneshwa na DSTV

Mchezo wa Yanga vs Kaizer Chiefs kuoneshwa na DSTV


Imefahamika kuwa mchezo wa Klabu ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa leo majira ya saa moja usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam hautarushwa na kituo cha Azam TV kwa Wananchi waliopo ndani ya mipaka ya Afrika ya Kusini.


Badala yake mchezo huo wa kuhitimisha Tamasha la "Siku ya Wananchi" utaoneshwa na DSTV na Azam Media wameridhia jambo hilo.


Ilikuwa ni kawaida miaka yote michezo ya Yanga katika kilele cha Tamasha la Siku ya Wananchi kurushwa na Azam TV pekee, lakini safari hii mambo ni tofauti na hasa ni kutokana na ujio wa timu ya Kaizer Chiefs.


Lakini kwa wakazi wa Tanzania na sehemu nyingine Duniani watauona mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa kupitia Azam TV.


Taarifa hiyo imetolewa na Klabu ya Yanga kama inavyosomeka kwa kirefu hapa chini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad