Kamati ya Uchunguzi ya Bunge la Seneti Nchini Kenya imeitaka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kumchunguza Gavana huyo wa zamani wa Jiji la Nairobi kutokana matumizi mabaya ya Fedha za Umma.
Sonko anadaiwa kuwalipa Maafisa 33 waliokuwa wakimlinda wakati akiwa Ziarani Jijini Mombasa mwaka 2018 huku Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ikibaini ubadhirifu mwingine wa Tsh. 248,101,265 zilizotumika katika Masuala ya Ulinzi wakati wa Uongozi wake.
Aidha, kamati hiyo imetaka Inspekta Jenerali wa Polisi ahojiwe na kutoa maelezo kwa kitendo cha kuruhusu Maafisa 33 wa Polisi kumlinda mtu mmoja.