Mimi si Mwendawazimu, Fiston Mayele yupo Yanga Kwa Mkopo - Jembe

 

Mimi si Mwendawazimu, Fiston Mayele yupo Yanga Kwa Mkopo - Jembe

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Mayele anaitumikia klabu hiyo kwa mkopo kutokea AS Vita Club ya nchini kwao Congo DR.


Kauli hiyo ya Saleh inajiri ikiwa kuna fukuto ndani ya Yanga ambapo uongozi wa klabu hiyo chini ya rais wao, Eng. Hersi Said wakipambana kumbakisha mfungaji bora wa NBCPL na CAFCC ambaye pia ni mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.


“Mayele kusema anapenda pesa, aongezewe pesa ili abaki Yanga, hivi Watanzania hatupendi hela? Anachokisema yupo sahihi lakini logically mkataba wa Yanga na Mayele unaisha mwaka 2024.


“Swali langu ni kwa nini Yanga wanahangaika kumbakiza? Uliwahi kusikia wapi mchezaji una mkataba naye wa mwaka mmoja unahangaika kumbakiza? Si unamuacha tu. Kama hutaki kumuuza unawaambia tu kwamba hutaki kumuuza.


“Mchezaji wako ambaye amebakiza mwaka mmoja halafu ukawa unahangaika kumbakiza asiondoka, maan ayake yule sio mchezaji wako asilimia 100. Mimi naendelea kusisitiza kwamba sio mwendawazimu, Mayele ni mchezaji wa mkopo Yanga.


“Kuna kipengele cha mkataba wake kinachoonyesha kwamba ikitokea timu imeleta ofa kubwa aruhusiwe kuondoka. Kwa hiyo Yanga ina kazi ya kumbakiza Mayele.


“Ningepewa nafasi ningewashauri yanga wambakize Mayele kwa sababu wanakwenda kucheza Champions League (CAFCL) ambayo ni ngumu kuliko shirikisho, huwezi kumwachia mshambuliaji ambaye ameimarika, Mayele wa msimu huu ni tofauti na wa msimu uliopita.


“Hata kama mtasajiri wachezaji wapya kumbuka wanahitaji muda ili kuweza kutengeneza muunganiko na wenzao na kufanya vizuri. Uzuri mwakilishi wake ni Jasmin ambaye ni Mtanzania, hivyo wanaweza kuzngumza vizrui na Mayele akaendelea kusalia yanga,” amesema Jembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad