Mimi namsapoti mume wangu kwasababu tumejenga nyumba 8 kupitia muziki, kwahiyo mimi nasapoti sana kazi yake kwasababu tunafanikiwa kupitia muziki wake, muziki unalipa na una hela. Zamani wanawake walikuwa wanampenda(kumpapatikia) sana Mr.Blue, yaani alikuwa wa moto kipindi kile kama alivyo Diamond Platnumz sasa hivi, ila namshukuru Mungu sasa hivi katulia"' amesema Waheeda Sylvester mke wa Mr.Blue
Waheeda aliwahi kuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2008 na kuingia top 10, pia aliwahi kuwa video queen kwenye nyimbo kadhaa za wasanii maarufu Bongofleva
Mr.Blue aliwahi kusema kwa mara ya kwanza yeye na mke wake huyo walikutana katika klabu ya usiku na hakudhania kuwa wangedumu kutokana na fikra zilizojengeka vichwani mwa wengi kuhusu kukutana na mtu maeneo ya starehe kisha kuanzisha mahusiano, lakini takribani miaka 14 sasa imepita wapo pamoja ikiwemo miaka yao ya kufunga ndoa humo humo, wamejaaliwa watoto 3
Mr.Blue alishasema kuwa mama yake alipomuona Waheeda akamwambia huyu mwanamke ni sahihi kwako, aidha, Blue alisema hata alipokuwa na makundi ya marafiki wasio sahihi na kupelekea kutumia mihadarati na kuhatarisha kazi zake za muziki, Waheeda alisimama kidete kumshauri aachane na makundi ya watu wasio sahihi yatampoteza na baada hawatokuwa msaada kwake
View all 5 comments
1 HOUR AGO