Baada ya kuibuka sintofahamu kuhusu kiungo huyo, Rais wa Heshima wa klabu hiyo @moodewji aliibuka na andiko la kuhoji kuhusu mchezaji huyo na kisha muda mfupi taarifa rasmi ikatolewa na klabu.
"Huyu mchezaji ambaye ana mkataba na timu kubwa, mbona analeta tabu, Simba ikiamua jambo imeamua".
Huku taarifa ya klabu iki sema "Tabu ipo pale pale kwa wapinzani. Clatous Chama na Fabrice Ngoma siku ya Ijumaa Julai 21, 2023 wataanza safari kwenda kwenye kambi yetu nchini Uturuki."