Leo @Luambano77 aliuliza swali kuhusu usajili unaofanywa na Simba, Azam, Yanga na Singida Fountain Gate kama unazingatia ushiriki wao wa mashindano ya kimataifa.
Lengend @AmriKiembaTZ akatoa majibu kwa kusema kila timu inasajili kwa kulingana na malengo iliyojiwekea.
“Inategemea na malengo waliyonayo kama timu ndipo tunaweza kusema wamezingatia au hawajazngatia kile ambacho wamekusudia kukifanya.”
“Kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ya namna yetu ya kusajili, badala ya kuleta tu mchezaji kwakuwa na passport ya nchi fulani, tumekuwa tukizingatia kwa wakati huo anafanya nini.”
“Kwa hiyo kwangu naona kuna mabadiliko kwenye eneo la usajili kwa maana ya kuleta wachezaji ambao wanakuja kuongeza kitu kwenye timu.”
“Mchezaji kufika na kushindwa kufikia matarajio ya watu ni jambo jingine lakini umesajili mchezaji wa aina gani ndio kitu ambacho najaribu kukiangalia.”
“Tumeona Aziz Ki kuna nyakati amekuwa akipata shida kwenye kiwango ‘form’ lakini daraja ‘class’ imemfanya bado awe mchezaji muhimu kwenye ligi yetu na timu yake.”