Mrembo Zaiylisa Afunguka Chanzo cha Ndoa yake na Dullah Makabila Kuvunjika Ndani ya Miezi Miwili


Zaiylisa amekiri ndoa yake na Dullah Makabila kumomonyokeana kwa talaka tatu huku akisema sababu kubwa ya kumchoka Dullah mapema ni kuwa mwingi wa matukio yasiyoisha na pia akieleza kuwa Dullah hajatulia na hata wakati anaolewa baadhi ya ndugu wa Dullah walimgusia hilo awe makini nae

Amesema miongoni mwa matukio ya Dullah ni kumfuma na sms za kinadada wa mjini mara kadhaa na akiuliza anaishia kumbulia vipigo akieleza pia kuwa Dullah ni mtu wa hasira sana

Zaiylisa ameeleza zaidi kwamba alionywa mapema kuhusu tabia za Dullah ila akaamua kuolewa nae hivyo amejitahidi sana ndoa yake kudumu kwa miezi miwili na siku kumi tu

Zaiylisa amesema licha ya Dullah kuwa mwingi wa matukio lakini kwa upande wake yeye Zaiylisa hakuwahi kumsaliti Dullah tangu wanafunga ndoa na hata Dullah mwenyewe alikuwa akishangazwa kutofuma sms zozote tata katika simu yake mkewe huyo

Kwa upande wa Dullah ambaye hata ndoa yake nyingine kabla ya hii haikudumu, awali alisema Zaiylisa ana tabia ya kumdharau hata mbele ya marafiki zake, ila alipoulizwa tena safari hii amesema asingependa kuongelea mambo ya kifamilia huku akidai bado anampenda mkewe lakini hata hivyo Zaiylisa amesema amemchoka Dullah na matukio yake hataki kuendelea na hiyo ndoa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad