Dansa na msanii maarufu Msami, ameweka wazi kile kilichowafanya waachane na muigizaji Irene Uwoya ambaye waliwah kuwa kwenye mahusiano miaka kadhaa iliyopita.
Msami amefunguka hayo alipokuwa anazungumzia maisha yake ya mahusiano kwenye kipindi cha mahusiano cha Wasafi FM kinachoongozwa na Diva.
"Mimi na @ireneuwoya8 hatukugombana...kila mmoja alikuwa busy ndio maana tukaachana...kuna wakati alikuwa anaingia kwenye masuala yake ya siasa na mimi pia niliamua tu kurudi nyuma kidogo.
"Kila mtu alikaa kimya na hakuna aliyemtamkia mwenzake kwamba penzi limeisha ila ndio tuliachana kwa staili hiyo. Pamoja na yote Uwoya ni mwanamke mwenye upendo na heshima sana," alisema Msami.