Mtibwa Sugar Wabeba Ubingwa Kwa mara ya Tano mfululizo LIGI ya Vijana

 

Mtibwa Sugar Wabeba Ubingwa Kwa mara ya Tano mfululizo LIGI ya Vijana
Mtibwa Sugar U20 Wakishangilia Ubingwa

Dakika 120 zimeweza kuamua ubingwa wa fainali ya ligi ya vijana chini ya miaka 20 na Mtibwa Sugar kufanikiwa kutetea ubingwa mara ya tano hii leo dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa Azam Complex Chamazi

Fainal hiyo ulimalizika kwa ushindi wa bao 1-0, Athuman Makambo akaifungia Mtibwa bao lake la Saba na kuibuka kinara wa mabao Ligi ya Vijana chini ya miaka 20.

Mtibwa Sugar yakomba kila kitu Ligi Kuu ya Vijana U-20, kuanzia Kombe la ubingwa, mfungaji bora, kipa bora na mchezaji bora.

Mfungaji Bora, Athuman Masumbuko 'Makambo' kafunga mabao saba, likiwemo lililowapa Mtibwa Sugar ubingwa tano mfululizo kwa kuilaza Geita Gold usiku huu ndani ya dakika za nyongeza

Kipa Bora Toba Kutisha na Mchezaji Bora ni Ladaki Chasambi aliyetetea kwani msimu uliopita aliibeba. Michuano hii ilianza 2008 na Mtibwa imebeba mara tano katika fainali tano mfululizo ilizoingia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad