Mwamba Anayedai Alikuwa Mpenzi wa Jeniffer Kanumba Afunguka "Alikuwa Hataki Watu Wajue"


Niliachana na Hanipha Jennifer Kanumna sababu hakutaka watu wajue mimi ni mpenzi wake - Peter Lubango

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Peter Lubango, amesema kilichomfanya aachane na mwigizaji Hanipha Daudi maarufu kama Jennifer Kanumba, ni kwasababu alikuwa hataki watu wajue kama wapo kwenye mahusiano.

Amesema alikuwa anampenda sana Jennifer, kuna siku ilikuwa siku ya birthday yake akamposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha akaandika "Naoa" akijua Jennifer ataifurahia post hiyo, lakini matokeo yake ni kwamba huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa penzi lao kumomonyoka kwani baada ya hapo Jennifer alim-block kila sehemu na huo ndiyo ukawa umauti wa penzi lao

Anasema alikuwa anajua kama mwenzake hapendi kupostiwa, alifanya hivyo kwasababu alikuwa anataka mapenzi yao yawe ya siri na alimposti makusudi akijua mwenzake atafurahi lakini haikuwa hivyo. Amesema alijiuliza mara kadhaa baadae akagundua pengine yeye alikuwa hapendwi bali zilipendwa pesa zake akaamua kutafuta penzi sehemu nyingine

Credit: FahariMedia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad