Mwimbaji mkongwe wa Uganda Jose Chameleone Afunguka Afya yake Baada ya Kuwa Hoi Marekani



Mwimbaji mkongwe wa Uganda Jose Chameleone hatimaye ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kulazwa kwa siku chache katika Hospitali ya Aline Medical katika jimbo la Minnepolis, Marekani. Habari kuhusu kulazwa kwake hospitalini ziliibuka siku chache zilizopita huku ripoti zikionyesha kuwa alikuwa akiugua maradhi ya tumbo.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, mwimbaji huyo wa Uganda aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na familia yake kwa kusimama naye katika kipindi ambacho alikuwa hospitalini. Chameleone pia alitoa shukrani kwa hospitali ya Marekani ambako alikuwa amelazwa kwa kumhudumia na akabainisha kuwa sasa yuko katika harakati ya kupona kabisa.

Pia alionyesha imani yake kwamba hivi karibuni atapata afya yake nzuri. “Ijapokuwa kupona kwangu bado kunaweza kuhitaji muda na subira, nina hakika kwamba nitarejea katika afya njema hivi karibuni. Mungu amekuwa mwema kwangu siku zote,” alisema. Wiki iliyopita, babake Chameleone aliiambia Bukedde TV kwamba nyota huyo mwenye umri wa miaka 44 amekuwa na matatizo ya tumbo.

“Chameleone amekuwa mgonjwa katika miezi iliyopita. Alipohamia Amerika, ugonjwa ulizidi kuwa mbaya. Sasa ni mgonjwa sana, yuko kwenye kitanda chake cha wagonjwa. Amekuwa akipata matatizo kwenye tumbo ambayo anapatiwa matibabu kwa sasa.” babake Chameleone alieleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad