Ndege za Air Tanzania Hatarini Kukamatwa


Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 [TZS bilioni 266] kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi uliochukuliwa wakati wa utawala wa Hayati Rais Dkt. John Magufuli mwaka 2018 wa kufuta leseni yao ya uchimbaji wa madini ya nikeli.

Kampuni hizo zilifungua kesi na kufanikiwa kuishinda Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka wajibu wake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Pamoja (BIT) kati ya Uingereza na Tanzania na sheria za kimataifa kwa kutaifisha leseni hiyo.

Tanzania pia imeamriwa kulipa dola milioni 3.859 [TZS bilioni 9.3] kama gharama za kisheria kwa walalamikaji, pamoja na ada na gharama za ICSID

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad