Ngoma avunja mkataba Sudan atue Simba




MWANASPOTI linajua kama mambo yataenda kama yalivyopangwa muda wowote klabu ya Simba itamalizana na kiungo Fabrice Ngoma baada ya kuvunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan.

Ngoma amesitisha mkataba na Al Hilal leo baada ya kushindwa kuwa na mwanzo mzuri na klabu hiyo akiwa majeruhi wa mara kadhaa.

Mwanaspoti linajua kiungo huyo yupo Dar es Salaam akisubiri barua yake ya kumalizana na Al Hilal ambapo wakati wowote anaweza kusaini Simba tofauti na ilivyozushwa kwenye mitandao ya kijamii akihusishwa na Yanga na Azam.

Simba imekuwa ikihitaji kiungo katika dirisha hili la usajili huku baadhi ya mabosi wa juu wa klabu hiyo kutua kwa Ngoma aje kuimarisha timu yao.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kiungo huyo anaweza kufanyiwa vipimo vya afya kwa siri leo ambapo endapo atafuzu atapewa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine.

Simba inataka kufanya maamuzi ya haraka kwa Ngoma kabla ya kumuingiza katika msafara wa timu hiyo kuelekea kambini nchini Uturuki tayari kwa maandalizi ya msimu mpya. Usilale. Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii Kwa habari za uhakika na usikose nakala Yako ya Mwanaspoti kesho Jumatano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad