Rosa Ree ni mmoja kati ya wanamuziki wakubwa wa Hip Hop nchini Tanzania. Hata hivyo, licha ya ufanisi kimuziki, Rosa Ree alipitia changamoto ya afya ya akili baada ya kujifungua mtoto wake.
Msanii huyo alikumbana na unyanyapaa mkubwa baada ya kujitokeza na kusema kwamba hayuko sawa hata kusababisha kupoteza kandarasi na mikataba kadhaa ya kufanya kazi.
"Fikiria mtu unapitia msongo wa mawazo ambao unakuja baada ya kujifungua, wanakupokonya zile kazi au ile mikataba ambayo ulikuwa nayo. Kwa sasa nimeanza kuizingatia afya yangu ya akili kwa umakini zaodi.
"Nahitaji kujiangali, kujitazama na kujizingatia upya, siwezi nikampenda mwenzangu kama sijipendi, nimepata msaada mkubwa sana kutoka kwa mashabiki zangu, wasanii wenzangu na Serikali,"