Padre Afia Guest Akidaiwa kuwa na Mwanamke Ambae ni Mpenzi Wake


Padre Afia Guest Akidaiwa kuwa na Mwanamke Ambae ni Mpenzi Wake
Padre Joseph Wanjiku




Kenya. Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya Ruai nchini Kenya amefariki dunia akiwa hotelini ikidaiwa kuwa alikuwa na mwanamke anayehisiwa kuwa ni mpenzi wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Capital News ya nchini humo imesema padri huyo aliyetambulika kwa jina la Joseph Wanjiku (43) alianguka na kufariki Jumamosi asubuhi ya Julai 8, akiwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake ambaye pia ni mfanyakazi wa kanisa hilo.

Inadaiwa Wanjiku alikodi Hoteli pamoja na mwanamke huyo iliyoko jimbo la Gatanga ambako walilala Ijumaa usiku.

Kulingana na ripoti ya polisi ilipofika asubuhi mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Ruth Karanja (32) alienda kituo cha polisi kutoa taarifa kuwa Wanjiku alikuwa amepatwa na kizunguzungu na kupoteza fahamu.


Polisi wanasema wafanyakazi wa hoteli hiyo walipomfuata Padri huyo walimkuta akiwa amepoteza fahamu na wakajaribu kumkimkimbiza katika hospitali ya karibu.

Walipofika hospitali walitaarifiwa kuwa Wanjiku alikuwa ameshafariki dunia. Sababu ya kifo haijaanzishwa.

"Uchunguzi wa kifo hiki umeanzishwa na uchunguzi wa maiti pia utafanywa. Maofisa wetu wamechukua taarifa kutoka kwa mwanamke ambaye alikuwa naye mara ya mwisho na wafanyakazi wa hoteli hiyo,” taarifa ya Polisi imeeleza.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad